Thursday, October 30, 2014

Tanzia nzito katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Mt. Agustino Cha Tabora (Archbishop Mihayo University College of Tabora-AMUCTA). Hayati (Happiness) aliyekuwa akisomea kozi Uhusiano wa Umma na Masoko katika mwaka wa Tatu (3) amekumbwa na umauti leo hii asubuhi katika hospitali ya Mirambo-Tabora. Hayati alikuwa anasumbuliwa na Typhoid pamoja na sickel cell. Imethibitishwa na moja ya mhadhiri wa chuo hicho alipoongea na mtandao huu kwa njia ya simu. Mtandao huu utaendelea kukupa taarifa zote za msiba huu. PIA TUNAUNGANA NA YEYOTE ALIYEGUSWA NA MSIBA HUU KATIKA MAOMBOLEZO. MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU PAHALA PEMA PEPONI

Friday, September 05, 2014

Namna mahitaji ya kihisia ya wenzi yanavyosababisha misuguano ya kimahusiano na ndoa PAMOJA na dini nyingi kubwa kupiga marufuku talaka kwa waumini wake, takwimu rasmi za Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) zinaonyesha kwamba talaka nchini zimeongezeka kwa asilimia 49 katika kipindi cha mwaka 2007 hadi 2009. Kwa upande wa Zanzibar pekee, tunaambiwa, asilimia 95 ya migogoro 1,753 ya ndoa iliyosajiliwa kwenye Mahakama ya Kadhi nchini humo iliishia kwa talaka. Hali inatisha, au sio? Katika hali halisi, shauri ya utamaduni wa kuyaonea aibu masuala ya kuachana, hali inaweza kuwa mbaya zaidi. Watu wengi wanaweza kuwa wanaugulia maumivu ya ndoa na kuamua ama kufa na tai shingoni, au kutafuta 'michepuko' ya hapa na pale katika jitihada za kupunguza maumivu. Katika nchi za Ulaya, ambako kidogo kuna uhuru wa mtu kufanya atakalo ikiwa ni pamoja na kuomba talaka, hali ni tete zaidi. Kwa mfano, tunaambiwa, wakati idadi ya ndoa zinazofungwa mwaka 2010 ilipungua kwa asilimia 39 barani humo, talaka zimeongozeka kwa asimilia 200 katika kipindi cha mwaka 1979 mpaka 2010. Takwimu hizi zinaonyesha namna taasisi ya ndoa inavyoendelea kupoteza umaarufu wake kwa kasi huku watoto wengi wakiendelea kuzaliwa nje ya ndoa. Katika nchi nyingi za Ulaya, asilimia zaidi ya 50 ya watoto wanazaliwa nje ya ndoa. Iceland oekee kwa mfano, asilimia ya watoto wanaozaliwa nje ya ndoa imefikia 66.9 mwaka 2012. Hapo hatujazungumzia mimba zilizotolewa pamoja na kukithiri kwa matendo ya uzinzi na uasherati ambayo ni matokeo ya michepuko ya wanandoa waliochoka maisha ya ndoa. Ingawa jambo hili limekuwa likifanyiwa utafiti tangu zamani, kwa sasa limeanza kuvutia hisia za watafiti wengi zaidi kufuatia ongezeko hilo la talaka. Jambo linalohitaji majibu ya hakika na makini ni kwamba iweje wapenzi wanaoanza mapenzi yao kwa msisimuko kujikuta katika hali ya kuchokana na hata kuachana katika kipindi kifupi? Kwa nini wapenzi waliooana kwa 'harusi ya kufa mtu', kwa furaha na nderemo za matumaini makubwa, wajikute wakizozana kwa hasira na uchungu, wakipigana, kupishana, kuchokana na hata kufikia kuhisi suluhu pekee ni ama 'kuchepuka', 'nyumba ndogo' au kuachana rasmi? Tumekosea wapi? Kwa nini ndoa inazidi kuwa taasisi iliyo kwenye hatari ya kupotea? Tafiti zinasemaje kuhusu mitazamo ya wanandoa wanaotengana? Utafiti uliofanywa na Amato na Previti na kuchapishwa kwenye Jarida la Masuala ya Familia mwaka 2003, unaonyesha kwamba watu wengi wanaachana kwa sababu ya hisia za kukosekana kwa uaminifu, wenzi kushindwa kuwasiliana, hisia za kukosekana mapenzi na hivyo wenzi kujikuta wakijisikia watu wasio na furaha tena na mengine mengi. Tafiti za awali zimefanya jitihada ya kujua sababu za kuchokana huko kwenye ndoa kwa kutazama makundi mbalimbali. Tukianza na jinsia, watafiti Levinger; Cleek & Pearson; Kitson; Bloom, Niles & Tatcher kwa nyakati tofauti walichunguza mitazamo ya wanaume na wanawake kuhusu sababu ya migogoro. Wanaume wanaorodhesha sababu kama vile wanawake kuwa wazinzi na kutumia muda mwingi kazini kuliko nyumbani, kukosekana mawasiliano baina ya wenzi, kubadilika kwa vipaumbele, kama sababu kuu. Wanawake kwa upande wao wanataja ulevi na uzinzi wa wenzi wao wa kiume; mwanaume kushindwa kuihudumia familia yake kifedha; udhalilishaji wa kihisia na kimwili hali inayosababisha furaha kutoweka na kutokuendana kitabia kama tatizo kuu. Kadhalika, tafiti nyingine zilizofanywa na Kitson, Levinger na Goode kwa nyakati tofauti, zimejaribu kutazama uwezo wa kifedha na elimu katika matatizo haya. Ndoa na mahusiano ni mada inayouza vitabu kwa wingi Picha msome zaidi bwaya
HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, KWA WANANCHI, WAKATI WA MAJUMUISHO YA MKOA WA DODOMA, TAREHE 04 SEPTEMBA, 2014 Utangulizi Mheshimiwa Dkt. Rehema Nchimbi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma; Waheshimiwa Mawaziri; Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya, Wabunge, Wenyeviti na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Miji; Waheshimwa Madiwani; Wazee Wangu; Ndugu wananchi; Kuna methali ya Kiswahili isemayo hakuna refu lisilokuwa na ncha. Hatimaye ziara yangu ya Mkoa wa Dodoma imefikia mwisho. Ziara hii niliyoianza tarehe 28 Agosti, 2014 imenifikisha kwenye wilaya zote za Mkoa wa Dodoma. Madhumuni ya ziara yangu yalikuwa kuona shughuli za maendeleo. Kuona tulipofanikiwa na pale ambapo pana matatizo tupatafutie ufumbuzi. Nimefarijika sana na hatua kubwa za maendeleo ambazo kila wilaya imezifikia. Nimejionea maendeleo makubwa katika sekta na nyanja mbalimbali za maisha ya wananchi wa mkoa huu. Hongereni sana. Aidha, nimeona au kusimuliwa kuhusu changamoto kubwa na ndogo zinazowakabili, ambazo zikiweza kupatiwa ufumbuzi ufanisi utaongezeka na kasi ya kujiletea maendeleo itakuwa kubwa zaidi. Elimu Natoa pongezi nyingi kwa viongozi na wananchi wa Mkoa wa Dodoma kwa juhudi kubwa mnazofanya na mafanikio mliyopata au mnayoendelea kupata katika kuendeleza elimu Mkoani kwenu. Kwa ajili hiyo basi idadi ya wanafunzi katika ngazi za awali, msingi na sekondari imekuwa kubwa kuliko wakati mwingine wo wote katika historia ya nchi yetu. Hivi sasa Mkoani Dodoma kuna wanafunzi wa Awali 47,427, wa Shule za Msingi 391,475 na wa Sekondari 59,035 ukilinganisha na wanafunzi wa Awali 55,524, wa Shule za Msingi 152,366 na wa Sekondari 24,288 mwaka 2007. Jukumu lililoko mbele yenu na mbele yetu pia ni kutatua matatizo yanayoikabili sekta ya elimu mkoani. Pamoja na kupanda kuliko ilivyokuwa mwaka 2012, kiwango cha ufaulu cha asilimia 38.2 kwa shule za msingi na asilimia 55.4 kwa shule za sekondari kwa mwaka 2013 ni chini ya wastani wa taifa wa asilimia 50.61 kwa shule za msingi na asilimia 58.25 kwa shule za sekondari. Hivyo mnayo kazi kubwa ya kufanya ili kufikia kiwango cha ufaulu cha asilimia 60 mwaka huu na asilimia 80 mwakani. Ongezeni bidii. Napenda kuwahakikishia kuwa sisi katika Serikali kuu tutaendelea kutimiza wajibu wetu kuhusu elimu. Tutaendelea kuleta walimu, vitabu na vifaa vya kujifunzia na kufundishia. Hali kadhalika tutaendelea kutoa pesa zitakazoboresha miundombinu ya shule na nyumba za walimu. Kwa upande wa walimu tumefanikiwa kutosheleza mahitaji ya walimu wa masomo ya sanaa kwa shule zote za sekondari. Kwa baadhi ya Wilaya kuna ziada ya walimu hao. Hii ndiyo hali ilivyo kote nchini. Hata hivyo, kuna upungufu mkubwa wa walimu wa sayansi jambo ambalo ni tatizo la kitaifa. Mkoa wa Dodoma una mahitaji ya walimu 4,076.Waliopo ni walimu 3,250, kati yao walimu 2,482 wa sanaa na 645 wa sayansi. Kuna jumla ya upungufu wa walimu 949 wa sayansi na ziada ya walimu 123 wa sanaa. Walimu wa ziada kwa masomo ya sanaa wapo Wilaya za Mpwapwa (34), Bahi (55), Dodoma Mjini (86) na Kongwa (92). Upungufu wa walimu wa sanaa upo Wilaya za Chamwino (103), Chemba (9), na Kondoa (32). Upungufu wa walimu wa sayansi upo wilaya zote. Hivi sasa kitaifa tuna pengo la walimu 23,500 na uwezo wa vyuo vyetu ni kuzalisha wanafunzi 2,500 kwa mwaka. Tumedhamiria kulikabili tatizo hili kwa nguvu zote na maarifa yetu yote. Sina wasiwasi kwamba tutafanikwia kama ilivyokuwa kwa changamoto nyingine nyinig. Kuhusu ujenzi wa maabara katika shule za Sekondari za Kata, narudia kuwakumbusha viongozi wa Wilaya na Mkoa wa Dodoma kwamba muda wa miaka miwili tuliopeana mwaka 2012 unaisha mwezi Novemba, 2014. Na, kupitia kwenu nawakumbusha viongozi wa Mikoa yote na Wilaya zote nchini ifikapo Novemba mwaka huu tutaulizana. Hatutaacha kubanana na kama hapana budi kuwajibishana. Tunaendelea kuboresha upatikanaji wa vitabu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari. Mpaka sasa uwiano wa kitabu kwa wanafunzi umefikia 1:3. Tutaendelea kutenga fedha zaidi ili kila mwanafunzi awe na kitabu chake. Suala la nyumba za walimu nalo ni jambo ambalo tunalipa umuhimu. Tunaendelea kuanzia mwaka wa jana kutekeleza mpango wa kuzipatia shilingi milioni 500kila Halmashauri kwa ajili ya ujenzi huo. Halmashauri za Wilaya ya Mkoa wa Dodoma zitaingizwa kwenye awamu zinazofuata na fedha pia zitaongezwa. Nimefurahishwa na utekelezaji wa mpango wa utoaji chakula cha mchana kwa wanafunzi mashuleni katika Wilaya za Chamwino, Bahi, Kondoa, Mpwapwa na Chemba. Huu ni mpango unaofadhiliwa na Shirika la Chakula Duniani (WFP). Hapa nchini Mpango wa Chakula wa WFP za Mikoa 4 ya Dodoma, Singida, Arusha na Manyara. Jumla ya shule 640 za mikoa hiyo zinafaidika na mpango huu upo katika Wilaya 16. Ni mpango mzuri ambao manufaa yake ni kuwaongezea watoto mazingira mazuri ya kufuatilia na kuelewa masomo. Hivyo, tuusimamie vizuri ufanikiwe. Ni vizuri viongozi wa Mkoa na kila Halmashauri mkajipanga vizuri ili mpango huu mzuri uweze kuwepo kila Wilaya na uweze kuendelea punde WFP watakapoacha kugharamia mpango huo. Maana jukumu la kuhakikisha lishe ya watoto wetu ni letu wenyewe. Mkoa wenu unakabiliwa na tatizo kubwa sana la watoto wanaoanza darasa la kwanza kutomaliza darasa la saba na wanaoanza kidato cha kwanza kutomaliza kidato cha nne. Tatizo hili lipo katika kila Wilaya. Takwimu za Mkoa zinaonesha kuwa kati ya wanafunzi 54,301 waliosajiliwa darasa la kwanza mwaka 2007, ni wanafunzi 39,387 tu ndiyo walifanya mtihani wa kuhitimu darasa la saba mwaka 2013. Hii ina maana kuwa wanafunzi 14,914 hawakufanya mtihani ambao ni sawa na asilimia 27.5. Na kwa upande wa sekondari, kati ya wanafunzi 16,023 walioandikishwa kidato cha kwanza mwaka 2010, ni wanafunzi 12,693 ndiyo waliofanya mtihani mwaka 2013. Wanafunzi 3,330 hawakufanya mtihani huo, sawa na asilimia 21. Idadi hii ni kubwa mno, haikubaliki. Haiwezi kuachwa kuendelea lazima ikomeshwe. Narudia kusisitiza agizo langu nililotoa mwezi uliopita kwamba, kuanzia sasa Walimu Wakuu na Wakuu wa Shule ni lazima watoe taarifa za mahudhurio ya wanafunzi kwa Maafisa Elimu wa Wilaya kila miezi mitatu. Maafisa Elimu wa Wilaya nao watalazimika kutoa taarifa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ambae nae atawasilisha kwenye vikao vya Baraza la Madiwani la Halmashauri mwezi mmoja baada ya kupokea taarifa hizo. Halmashauri hazina budi kuchukua hatua stahiki, kijamii na kisheria, kuhakikisha kuwa watoro wanarudi shuleni. Wazazi wa watoto hao au mtu ye yote atakayebainika kuhusika na utoro huo abanwe ipasavyo. Maji Kama mjuavyo, kuwapatia wananchi wa Tanzania maji safi na salama karibu na wanapoishi ni moja ya malengo ya msingi ya Sera na shughuli za serikali na Chama tawala. Katika ziara yangu nimeshuhudia utekelezaji wake. Nimeweka mawe ya msingi ya ujenzi wa miradi ya maji na nimezindua miradi ya maji iliyokamilika. Jitihada zetu hizo zimetuwezesha kuwapatia maji asilimia 75.4 ya wakazi wa Mijini na asilimia 50.6 ya wakazi wa vijijini mkoani Dodoma. Lengo la kitaifa ni kuwapatia maji asilimia 90 ya wakazi wa mijini na asilimia 65 ya wakazi wa vijijini ifikapo 2015. Kwa hapa Dodoma kiwango hicho cha upatikanaji maji kina maana ya kufanya kazi ya ziada ili kuweza kufikia lengo. Miradi inayoendelea kutekelezwa sasa mijini na vijijini hapa Mkoani itakapokamilika itawezesha kufikia lengo. Rai yangu kwa viongozi ni kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo ikamilike kwa wakati ili wananchi wapate maji safi na salama mapema. Vile vile, nawaomba kusimamia na kuwaelimisha wananchi juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji na mazingira kwa ujumla wake. Viongozi, waache kulalamika juu ya uharibifu wa mazingira na vyanzo vya maji. Sheria zipo, mamlaka mnayo chukueni hatua ili kulinusuru taifa letu dhidi ya uharibifu wa mazingira. Umeme Tumeongeza, maradufu, juhudi za kuzalisha, kusafirisha na kusambaza umeme nchini. Shabaha yetu ni kuwawezesha asilimia 30 ya Watanznaia waweze kupata umeme ifikapo mwaka 2015. Tayari tumeshavuka lengo hilo kwa kufikia asilimia 36. Kwa Mkoa wa Dodoma katika mwaka huu wa fedha shilingi bilioni 43.8 zimetengwa kwa ajili ya kusambaza umeme vijijini. Fedha hizi zitawezesha zaidi ya vijiji 193 kupatiwa umeme katika Mkoa huu. Kila Wilaya niliyoitembelea kuna miradi kadhaa ya umeme inayoendelea kutekelezwa. Ndugu zetu Wilaya ya Bahi walinilalamikia kuwa wao wamepewa vijiji vinne tu. Nikawasiliana na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ambae ameahidi kuwa watafanya masahihisho stahiki. Maombi yangu kwa viongozi wenzangu wahimizeni wananchi waunganishe umeme majumbani na kwenye shughuli zao za kiuchumi na kibiashara. Barabara Ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli, viwanja vya ndege, bandari, umeme na simu ni mambo tuliyoyapa kipaumbele cha juu. Nilisema hivyo katika hotuba yangu ya kwanza tarehe 30 Desemba, 2005 na kurudia katika kupindi chote cha uongozi wangu mpaka sasa. Kwa upande wa barabara lengo letu ni kuunganisha mikoa yote kwa barabara za lami na kuimarisha baraba za mikoa, wilaya na Vijiji ziweze kupitika wakati wote. Katika ziara yangu ya Mkoa wa Dodoma nimeshuhudia mafanikio makubwa ya utekelezaji wa lengo hilo. Nimeweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya lami kutoka Mayamaya hadi Bonga. Hali kadhalika, nilizindua kukamilika kwa ujenzi wa barabara ya lami kutoka Dodoma hadi Fufu. Nimeambiwa kuwa zimebaki kilometa 25 kwa upande wa Fufu hadi Iringa ili kukamilisha ujenzi wa barabara yote ya Iringa hadi Dodoma yenye urefu wa kilometa 260 kwa kiwango cha lami. Bila ya shaka mtakubaliana name kuwa ujenzi wa barabara ya Dodoma – Babati unatoa fursa ya iana yake kwa maendeleo ya mji wa Dodoma na Mkoa huu kwa jumla. Jipangeni kuitumia fursa hiyo. Kule Kongwa niliweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya lami kutoka Mbande, Kongwa hadi Mpwapwa na Kibakwe. Napenda kurudia kuwatoa hofu ndugu zangu wa Mpwapwa na Kibakwe kuwa ujenzi wa barabara ile unaendelea na ndiyo maana pale njia panda ya Kongwa tulifanya shughuli za kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Mbande, Kongwa, Mpwapwana siyo uzinduzi wa barabara ya lami kutoka pale hadi Kongwa. Nimefarijika sana kuona jinsi barabara za mkoa na Wilaya zikiendelea kuimarishwa. Kwa kweli ilikuwa jambo la faraja kubwa kwangu kusikia kuwa vijiji vyote vya mkoani vinafikika kwa barabara. Ni ushindi mkubwa. Napenda kuwaahidi kuwa tutaendelea kuwapatia fedha kutoka Mfuko wa Barabara ili mzidi kuziimarisha barabara zenu. Bahati nzuri Mfuko huo tumeuongezea sana uwezo wake kutoka shilingi bilioni 56.1 mwaka 2005/2006 hadi shilingi bilioni 751.7 hivi sasa. Tulipokuwa wilayani Mpwapwa niliweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja jipya la Gulwe linalounganisha majimbo ya mpwapwa na Gulwe. Tulipokuwepo pale palijitokeza mawazo mazuri kuhusu namna ya kuikinga reli ya kati ambayo imekuwa inaharibiwa mara kwa mara wakati wa mvua katika maeneo ya Godegode, Gulwe, Msagali na Kilosa. Ulitolewa ushauri kwamba kama yakijengwa mabwawa katika mito inayovuka reli hiyo katika maeneo hayo. Mabwawa hayo yatapunguza wingi na kasi ya maji hivyo kuinusuru reli. Nilivutiwa na mawazo hayo na kuufikisha ujumbe kwa Waziri wa Uchukuzu Mheshimiwa Harrison Mwakyembe ambaye aliniambia kuwa ni jambo linalofanyiwa kazi. Nilizungumza pia na Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Pinda asimamie kuhakikisha kuwa jambo hili muhimu linafanyika. Tulikubaliana kuwa Wizara ya Maji, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika nao washiriki katika mpango huu kwani ni wadau muhimu wa mabwawa hayo. Hali kadhalika viongozi wa Mikoa ya Morogoro, Dodoma na Manyara wahusike. Natambua kuwepo maombi ya kutaka barabara kadhaa za Wilaya ziwe za mkoa ili zisimamiwe na TANROADS. Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa John Magufuli amesikia na zipo baadhi ambazo amezitolea majibu ya kukubali na nyingine anaendelea kutafakari nini afanye. Bila ya kuingilia atakachoamua napenda kusisitiza kuwa msingi mkuu unaoifanya barabara kuwa ya mkoa na hivyo kushughulikiwa na TANROADS ni kuunganisha Wilaya moja na nyingine. Barabara inayoanzia na kuishia ndani ya Wilaya haina sifa hiyo hata kama ni ndefu kiasi gani. Nalisema hili kwa sababu umeanza kuzuka mtindo wa Halmashauri kutaka kukwepa wajibu wao. Pale ambapo wamezidiwa ujuzi na uwezo waseme TANROADS itawasaidia lakini wasikwepe majukumu yao. Kilimo na Mifugo Masoko ya Mazao ya Kilimo Viongozi, Wazee wangu na Ndugu Wananchi; Hongereni kwa mafanikio mliyopata mwaka huu katika kilimo. Mkoa umezalisha tani 687,122 za mazao ya chakula wakati mahitaji yenu ni tani 494,331. Hivyo kuna ziada ya tani 192,791. Hiki ni kielelezo tosha kwamba juhudi zenu za kuleta mageuzi ya kilimo zinafanikiwa. Mkoa wenu una zaidi ya matrekta makubwa na madogo 1,756. Kati ya matrekta hayo Wilaya ya Kongwa ina matrekta 728. Hongereni sana na endeleeni kuongeza matumizi ya zana bora na pembejeo za kisasa za kilimo mpate mafanikio makubwa zaidi. Nilipoingia mkoa huu kutokea mkoa wa Morogoro kilio kikubwa cha wakulima kilikuwa soko la mahindi kwa maana ya kukosekana mnunuzi anayetoa bei nzuri kwa wakulima. Wapo watu binafsi wanaonunua mahindi ya wakulima kwa bei ndogo sana. Kilio hicho nilikikuta Mkoa wa Morogoro na Tanga kabla ya hapo. Nilizungumza na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mheshimiwa Mhandisi Chiza kuhusu jambo hilo. Akamtuma Katibu Mkuu Mama Sofia Kaduma na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula Ndugu Walwa waje kujiunga na msafara. Ndugu Walwa alieleza kuwa walichelewa kuanza ununuzi katika ukanda wa kati lakini sasa wako tayari kufanya hivyo. Ni matumaini yangu kuwa hatua hiyo italeta nafuu kwa wakulima. Naomba tufanye kazi kwa karibu na NFRA tuwasaidie panapobidi ili wafanikishe jukumu lao. Ni jambo lenye maslahi kwa wakulima, kwa Wakala na Taifa kwa jumla. Migogoro ya Wakulima na Wafugaji Wazee wangu; Nilipokuwa Kibaigwa, Kongwa nilipokea malalamiko yenye mvumo mkubwa kutoka kwa ndugu zetu wanaofanya shughuli za kilimo katika Wilaya ya Kiteto. Wanalalamikia kufukuzwa, kupigwa, kuuawa, kuchomewa moto nyumba, matreka na kuporwa na kunyang’anywa mali zao na ndugu wa jamii ya wafugaji. Wapo waliokuwa wanadai kuwa walikuwa wanaishi huko kwa zaidi ya miaka thelathini hivyo kujikuta wanaambiwa ondoka, nyumba zinachomwa moto, mali zinaharibiwa ni mambo magumu sana kuelewa. Nilipokuwa Mkoa wa Morogoro nilipokea malalamiko kutoka kwa wakulima dhidi ya wafugaji kwamba mifugo imekuwa mingi mno kupita kiasi na kwamba wanaharibu mazao ya wakulima. Nilipokuwa Morogoro nilisema mambo ambayo ningependa kuyarudia tena leo. Kwanza, kwamba, ardhi hainongezeki lakini watu wanaongezeka na shughuli zinazohitaji kutumia ardhi zinaongezeka. Kwa sababu hiyo wanadamu hawataweza kufanya kila kitu anachotaka katika ardhi hiyo hiyo aliyonayo. Hivyo analazimika kupanga matumizi bora ya ardhi. Yaani anatakiwa kupanga atafanya nini, wapi katika ardhi yake. Kwa ajili hiyo nimewataka viongozi wa vijiji, Wilaya na Mkoa kuwa na mpango wa matumizi ya ardhi kwa shughuli mbalimbali katika maeneo yao ya uongozi. Kwa upande wa ardhi inayotengwa kwa ufugaji hawana budi kujua ina uwezo wa kubeba mifugo mingapi na ya aina gani. Mgao huo ukishafanywa lazima usimamiwe kwa dhati. Ikifanyika hivyo mtakuwa na hakika na kila hatua ya maendeleo inayochukuliwa na kuepusha migogoro kati ya wakulima na wafugaji. Hapatakuwa na migogoro kwa sababu kila mmoja atakuwa na eneo lake la kutosha kufanyia shughuli zake. Pia hapatakuwa na migogoro kwa vile baada ya ukomo wa uwezo wa mifugo inayoweza kubebwa na ardhi iliyotengwa kujulikana na kuzuia mifugo zaidi isiruhusiwe kuingia. Najua wakati mwingine wenye mifugo wakiambiwa hivyo wanaona wanabaguliwa na kunyimwa haki yao kama raia. Si hivyo, hawajanyimwa haki ya uraia ya kuishi po pote upendapo. Kilichofanyika ni kuweka utaratibu mzuri wa raia kutumia haki yake hiyo kwa manufaa yake na jamii yote. Inampa fursa za uhakika kustawisha mifugo yake na kumuepusha na ugomvi na wengine. Jambo la pili, nililolisisitiza kule Morogoro ambalo napenda kulirudia tena hapa leo ni kuwa ndugu zetu wanaofuga wahakikishe kuwa mifugo yao haili mazao ya wakulima. Kwa kweli jambo kubwa linalozua chuki, uadui na ugomvi baina ya wakulima na wafugaji ni mifugo kula mazao ya wakulima shambani. Kama hili halitokei sioni mazingira ya kuwepo mgogoro kati ya wakulima na wafugaji. Kila mmoja ataendelea na shughuli zake na kuwa rafiki wa mwenzake. Nilipokuwa Morogoro niliwaomba wafugaji wapitishe azimio kuwa mwaka huu hakuna hata robo eka ya shamba itakayoliwa na kuteketezwa. Ikiwa hivyo, sidhani kama kutakuwa na mgogoro kati ya wakulima na wafugaji. Kuhusu yaliyotokea Kiteto kati ya wakulima na wafugaji nalo ni suala la uhusiano na uongozi. Kama watu wameishi huko na kufanya shughuli zao kwa zaidi ya miaka 30 kuna namna bora zaidi za wao kuondoka au kuwaondoa. Viongozi wanayodhamana kubwa ya kuona kuwa watu wa nchi hii hawafanyiwi vile. Nimezungumza na Waziri Mkuu ili tuangalie uwezekano wa mkutano kati ya viongozi wa Mikoa ya Manyara, Morogoro na Dodoma inayojumuisha Wilaya za Mpakani wakutane na kuzungumza namna ya kuondoa uadui na kuwafanya watu waishi pamoja na kushirikiana. Afya Nawapongeza kwa hatua kubwa mliyopiga katika kuboresha sekta ya afya kwa kupeleka huduma karibu zaidi na wananchi. Mkoa wa Dodoma una mtandao wa hospitali 8, vituo vya afya 41 na zahanati 316. Nafurahishwa pia na jitihada za kuwashirikisha wananchi katika ujenzi wa zahanati na vituo vya afya vipya ili kutimiza azma yetu ya kusogeza huduma za afya ndani ya eneo la mzingo wa kilometa 5 wanapoishi wananchi. Huko nyuma niliagiza kwamba kila Halmashauri ya Manispaa, Mji na Jiji ambayo iko Makao Makuu ya Mkoa, ijenge hospitali yake ili kuiwezesha hospitali ya Mkoa kufanya shughuli za rufaa za Mkoa. Manispaa ya Dodoma mko nyuma katika kutekeleza agizo langu hili. Tengeni eneo la ujenzi wa hospitali ya Manispaa na wekeni kwenye bajeti yenu ili tuijenge. Pia upo wajibu wa kisera kuhakikisha kuwa kila Wilaya ina hospitali ya Wilaya. Katika Mkoa wa Dodoma Wilaya za Kongwa, Bahi, Chamwino, Chemba na Dodoma Mjini hazina hospitali za Wilaya. Nimewataka waanze ujenzi wa hospitali hizo. Waweke mahitaji yao kwenye mipango ya maendeleo ili itafutiwe fedha. Nawapongeza kwa jitihada mnazofanya za kuhamasisha akina mama kujifungua katika zahanati, vituo vya afya na hospitali. Taarifa yenu inaonesha kwamba asilimia 79 ya akina mama wajawazito wanajifungulia katika vituo vya kisasa vya kutoa huduma ya afya na chanjo ya watoto mmefikisha asilimia 96. Msibweteke ongezeni uhamasishaji ili akina mama wote wajifungulie kwenye vituo vya afya na watoto wote wapate chanjo. Kwa ajili hiyo, napenda kushauri kuwa ujenzi wa sehemu ya akina mama wajawazito kusubiria kabla ya kujifungua (maternity waiting homes) ufikirieni kwa uzito unaostahili. Wenzenu wa Morogoro wamelifanya kuwa sehemu ya mipango yao ya kuendeleza afya ya akina mama wajawazito. Inasaidia kuokoa maisha ya mama wajawazito kunaweza kusaidia Mkoa huu pia na kwingineko nchini. Aidha, tuendelee kuhimiza mapambano dhidi ya ugonjwa ya UKIMWI katika maeneo yetu. Japo takwimu zinaonyesha kuwa maambukizi ya UKIMWI kimkoa yanapungua toka asilimia 3.4 mwaka 2008 hadi asilimia 2.9 mwaka 2012, lengo letu ni kutokuwa na maambukizi mapya kabisa. Ongezeni juhudi ili lengo letu hilo tulifikie. Nawapongeza pia kwa kuvuka lengo letu la kuhakikisha kwamba asilimia 30 ya Watanzania wanajiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii ifikapo 2015. Ninyi mmekwishafikisha asilimia 47.9. Hata hivyo, ziko Wilaya kama za Kondoa, Chemba na Manispaa ya Dodoma ambazo ziko chini sana. Ongezeni jitihada ili wananchi wengi zaidi wapate huduma ya mfuko huo. Ugonjwa wa Ebola Ndugu wananchi; Tangu mwezi Aprili, 2014 nchi za Afrika Magharibi hususan nchi ya Guinea, Siera Leone, Liberia na Nigeria zimekumbwa na mlipuko mkubwa wa ugonjwa hatari wa Ebola. Taarifa za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonesha kuwa tayari watu 3,500 wameambukizwa na tayari zaidi ya vifo 1,900 vimetokea. Asilimia 40 ya vifo hivi vimetokea ndani ya wiki tatu hadi kufikia tarehe 3 Septemba, 2014. Ebola ndiyo virusi hatari zaidi duniani kuliko hata UKIMWI. Ndiyo maana Shirika la Afya Duniani limeutangaza ugonjwa huu kuwa ni janga la dunia, na inatarajiwa athari zake zinaweza kuongezeka. Ugonjwa huu husababishwa na virusi vya Ebola na husababisha wagonjwa wengi kufa kwa vile ugonjwa huu hauna tiba maalum wala chanjo. Wataalam wanatuambia kwamba virusi vya Ebola hubebwa na ndege aina ya popo na wanadamu huupata kupitia kwa wanyama walioambukizwa kwa kuwagusa au kuwala. Wanyama hao ni pamoja na sokwe, nyani na swala. Maambukizi kutoka kwa mgonjwa huenda kwa mtu mwingine kwa kugusa damu au majimaji kutoka mwilini mwa mtu aliyeambukizwa ugonjwa huo au kwa kugusa maiti ya mtu aliyekufa kutokana na ugonjwa huo. Ugonjwa huu ni hatari sana kiasi kwamba hata watoa huduma za afya kama madaktari na wauguzi kama hawakuchukua tahadhari zinazotakiwa wanaweza kuambukizwa na hata kufa. Mpaka hivi sasa Daktari mmoja aliyekuwa anawahudumia wagonjwa wa Ebola kule Liberia amekufa. Dalili za ugonjwa huo ni pamoja na mgonjwa kuwa na homa kali ya ghafla, kulegea mwili, kuumwa na kichwa, kuumwa na misuli na kutokwa na vidonda kooni. Dalili hizi zinaweza kuambatana na kutapika, kuharisha, kutokwa na vipele, kutokwa na damu ndani na nje ya mwili na kushindwa kufanya kazi kwa figo na ini. Dalili za ugonjwa huu hujitokeza katika siku 2 hadi 21 baada ya kuambukizwa. Tunamshukuru Mungu kwani mpaka sasa hapa nchini hajapatikana mtu yeyote mwenye ugonjwa huu. Pamekuwepo na wagonjwa wanne waliohisiwa kuwa na Ebola ambao uchunguzi ulionesha hawakuwa na ugonjwa huo. Watatu kati ya wagonwja hao walikuwa ni wagonjwa wa malaria na mmojauchunguzi wake bado unaendelea. Wagonjwa wawili ni kutoka Dar es Salaam na wawili ni kutoka Geita na Nkasi. Wagonjwa hawa waliohisiwa walihudumiwa na walifanyiwa uchunguzi kwa kufuata tahadhari zote za ugonjwa wa Ebola. Hii imeonesha utayari wetu wa kukabiliana na janga hili. Pamoja na kutokuwepo kwa mgonjwa yeyote aliyehisiwa au kuthibitika kuwa na ugonjwa huu. Tumejipanga vizuri kuzuia ugonjwa huu usiingie nchini. Tumechukua tahadhari na kujiandaa vilivyo kukabiliana na janga hili kwa kuchukua hatua zifuatazo: (i) Tunacho Kikosi Kazi cha Taifa kinachoongozwa na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Donald Mbando cha kukabiliana na ugonjwa huu katika ngazi ya taifa hadi Wilaya. (ii) Tumekamilisha mpango wa kitaifa “Ebola Contingency Plan” na tumetenga Shilingi milioni 500ikiwa ni fedha za awali za utekelezaji wa mkakati huo. (iii) Tumeshaagiza Timu za Maafa za mikoa na wilaya kutekeleza mpango huo. (iv) Tumesambaza vifaa “personal protective equipment” kwa watumishi wa afya katika mikoa yote, wilaya zote, hospitali zote za Rufaa na kanda 37, viwanja vya ndege vya Julius Nyerere, Kilimanjaro, Mwanza na Zanzibar. Tumesambaza pia dawa. (v) Tumetenga kituo maalum tengefu (isolation unit) cha Wilaya ya Temeke na vituo vingine tengefu mikoani. (vi) Tumechukua tahadhari kubwa kwenye viwanja vya ndege. Tumekwishafunga mitambo maalum ya vipima joto na dalili za wagonjwa wa Ebola katika viwanja vya Mwalimju Nyerere (2), Mwanza (1), Zanzibar (1) na kituo cha Namanga (1). Tumeagiza pia scanners 5 ambazo zimekwishawasili na zitafungwa katika viwanja vyetu. (vii) Tumetoa mafunzo kwa watumishi wa afya wa mipakani na viwanja vya ndege. Tumetoa mafunzo hayo kwa watumishi 100 wa Dar es Salaam na 45kutoka mikoa ya Arusha, Kagera, Rukwa, Mwanza, Kilimanjaro, Kigoma na Zanzibar. Tumepeleka watumishi watatu nchini Jamhuri ya Kongo kupata mafunzo maalum. (viii) Tumeanza maandalizi ya kuboresha maabara zetu ili tuweze kufanya uchunguzi wa sampuli hapa hapa nchini. Kwa sasa, eneo zima la Afrika Mashariki tunategemea na tunatumia maabara ya Nairobi. Viongozi wa ngazi zote hizi wamepatiwa mwongozo wa utekelezaji. Tunachoomba ni ushirikiano wa wananchi wote katika kuchukua tahadhari na kutoa taarifa mapema iwezekanavyo mara tu mnapogundua dalili za ugonjwa huu kwa mtu ye yote. Mchakato wa Katiba Nilipozungumza na Taifa mwishoni mwa mwezi Julai, nilizungumzia mchakato wa Katiba. Nilielezea utayari wangu wa kufanya kila liwezekanalo kusaidia kufanikisha mchakato wa Katiba unaonndelea sasa. Kwa moyo huo, sikusita, nilipoombwa na Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia (Umoja wa Vyama vyenye Uwakilishi Bungeni) Mhe. John Momose Cheyo kukutana nao na kufanya mazungumzo ya mashauriano. Kama mnavyojua tulikutana tarehe 31 Agosti, 2014 Mjini Dodoma. Tumekuwa na mazungumzo mazuri. Tumepeana kazi ya kufanya na tumekubaliana kukutana tena tarehe 08 Septemba, 2014 kuendelea na mazungumzo yetu. Kinachotia moyo ni ule ukweli kwamba kila upande umeonesha kiu na utayari wa kuzungumza. Tuyape nafasi mazungumzo haya yatutoe hapa tulipo na kutusogeza mbele kwa umoja na mshikamano. CDA Mwisho, suala la CDA: Wakati wa kuzundia barabara ya Dodoma – Fufu Mbunge wa Dodoma Mheshimiwa Malole alielezea kwa uchungu matatizo ya CDA. Nimewaagiza Wadau wakae tutakutana tarehe 07 Septemba, 2014 tupokee ushauri. Naomba muwe na subira. Hitimisho Wazee wangu; Narudia tena kuwashukuru ndugu zangu wa Dodoma kwa mapokezi mazuri na ratiba nzuri iliyonipa nafasi ya kujifunza mengi kuhusu mkoa wenu. Naondoka nikiwa na kumbukumbu ya mambo mazuri yanayoendelea kufanyika hapa mkoani kuinua hali za maisha ya wananchi. Tafadhali ongezeni bidii. Mimi na wenzangu Serikalini tutaendelea kuwaunga mkono. Asanteni sana kwa kunisikiliza.
1. Maisha yako yanaweza kubadilishwa kwa muda mfupi na mtu hata usiemjua. 2. Watu wenye furaha pengine hawana kila kitu cha kuwapa furaha ila kile kidogo walichonacho hukipa maana ya kukifurahia. 3. Wapenzi wawili wanapogombana haimaanishi hawapendani,vivyohivyo wasiogombana haimaanishi wanapendana. 4. Unaweza kufanya jambo fulani la muda mfupi lakini likakunyima furaha milele . 5. Unapoagana na uwapendao waache na maneno mazuri pengine inaweza kuwa mara yako ya mwisho kuwaona. 6. Inaruhusiwa kuwa na hasira ila haimaanishi uwe katili. 7. Ukomavu wa mtu huja kutokana na changamoto alizozipitia kwenye maisha na kujifunza kupitia changamoto hizo na sio umri aliouongeza. 8. Wakati mwingine inatosha kusamehewa na wengine,ifike mahali ujifunze kujisamehe mwenyewe. 9. Sio lazima uwe na kiherehere cha kujua siri flani pengine kuijua kunaweza kubadili maisha yako milele. 10. Watu wawili wanaweza kutazama kitu kimoja lakini kila mmoja akaona tofauti.

Friday, April 12, 2013

NI WIKI YA MAJONZI MAKUBWA KWA KIFO CHA JOSEPH LEOPORD RWEYEMAM

ilikuwa jumamosi tarehe 6 april 2013 nilipopokea simu iliyo haribu siku yangu.ilikuwa ni simu ya kunitaarifu kuhusiana na ajali iliyotekea mkoani shinyanga maeneo ya kahama na ikinitaka kufuatilia na kujua wahusika katika ajali hiyo wana hali gani, kutokana na umbali niliokuwapo kufika eneo la tukio ilinilazimu kutafuta jamaa yangu aliekuwa kahama na kumuomba afuatilie habari hii, kwakweli habari nilizokuja letewa toka kwa rafiki yangu huyo hazikuwa na matumaini baada ya kunambia mtu mmoja aliyekuwa ajali hiyo amefariki na wengine wamejeruhiwa vibaya. huo ndo ulikuwa mwisho wa uhai wa ndugu yetu na rafiki yetu JOSEPH RWEYEMAM. nakumbuka mwaka 2008 kwa furaha kubwa nilipost hapa harusi yake na leo kwa huzuni kubwa na post habari ya kifo chake. tulikupenda joseph lakini Mungu alikupenda zaidi. R.I.P Joseph Rweyemam

Tuesday, November 29, 2011

“POSHO SI DHAMBI , DHAMBI NI POSHO INAPOKOSA UTU” - LEMA


Nimetafakari sana niliposoma kwenye magazeti kuwa sisi wabunge tumeongezewa posho bila hata sisi kufahamu jambo hilo .
Na kila mtu ametoa maoni mbali mbali juu ya jambo hili , ni kweli ni msimamo wa chama chetu (Chadema) kupinga posho mbali mbali zisizokuwa na tija na tulikubaliana hivyo kwenye vikao vya Chama Chetu vya Wabunge na kupinga mfumo wa posho uliopo kwa sasa ni msingi sahihi wa Chama kuonyesha hisia na ubadhilifu mkubwa unaotokana na ulipwaji mbaya wa posho kama ambavyo imejitokeza mara nyingi na hata hivi karibuni tumeshuhudia madudu mengi kwenye ripoti ya kamati ndogo ya Bunge iliyomchunguza Jairo. Lakini suala hili haliwezi kuepukwa kabisa na Chama kinajua ila utaritibu wa ulipwaji posho kwa watumishi mbali mbali wa umma ni tatizo kubwa na kuna mapungufu mengi sana ndio maana kupinga posho haina maana tu ya kupinga kiwango cha pesa anachopokea Mbunge au mtumishi yeyote wa UMMA bali mfumo mzima wa sera ya posho ili uweze kuwa na tija na kupunguza mianya ya wizi katika mfumo huu ambao umekuwa ukitumika vibaya kuliibia Taifa.

Pengine sisi wabunge ni vyema tukatambua kwanini wananchi wanapiga kelele kuhusu posho nilishawahi kusema Bungeni wakati nachangia kwenye Wizara ya Ustawi wa Jamii kuwa mshahara wa Wabunge , posho mbali mbali za Wabunge pamoja na marupurupu mengine yanaonekana kuwa anasa pale watumishi wengine wa serikali kama Manesi ,Asikari Magereza,Polisi ,Makarani Mahakamani wanapolipwa chini ya shilingi laki mbili na nusu kwa mwezi na wakati huo huo wanasikia mwakilishi wao akipiga kelele Bungeni kuwa posho ya laki mbili kwa siku ni ndogo. Ndio maana nimesema “POSHO SIO DHAMBI ILA POSHO NI DHAMBI PALE POSHO INAPOKOSA UTU , Na hapa lazima kutokee ugomvi wa kimasilahi na mgogoro mkubwa kati ya mwakilishi na anaye wakilishwa.

Pengine masilahi anayopata Mbunge ni ya kawaida sana tena sana ila yanaonekana kuwa anasa pale ambapo yeye kama mwakilishi anapolipwa kiwango cha posho cha siku moja ambacho ni sawa na mshahara wa mpiga kura wake kwa siku thelasini. Mimi nafikiri namna peke ya wabunge kutetea masilahi yao bora kwanza ni kupigania masilahi ya wapiga kura wote Tanzania na tukifanya hivi kama Wabunge hakuna Mwananchi hatakayeshangaa kwanini Mbunge awe na masilahi bora kwani ubunge ni nafasi kubwa pia inayositahili heshima kubwa kwani ni uwakilishi katika jamii.

Ebu jiulize wananchi wanaposikia Wabunge wamepewa milioni tisini kununua magari na wakati huo huo serikali imenunua bajaji kuwa ndio magari ya kubeba wakinamama wajawazito yaani (Ambulance) ni wazi kabisa wabunge wataonekani ni watu katili na walioenda bungeni kwa masilahi binafsi japo kuwa ukweli unabaki kuwa Wabunge wanahitaji magari imara na mazuri. Lakini Wabunge kama watafikiri Bajaj ni sawa kuwa gari la wakinamama wajawazito na wao kuchukua milioni tisini kwa magari ya binafsi bila kupiga kelele na kukataa unyanyasaji huu kwa wakina mama na Wagojwa ,hivyo ni dhahiri kuwa ugomvi hapa katika posho na masilahi ya Wabunge utasababishwa na tofauti ya masilahi dhidi ya wale waliowachagua kuwatetea ,Hivyo namna pekee Mbunge anaweza kutetea masilahi yake bora bila kuingiliwa na na kubugudhiwa ni Mbunge kuanza kufikiria masilahi ya watu wengine ambao pia ni watumishi wa UMMA ambapo yeye ni mwakilishi wake .

Nafahamu kuwa pamoja na kupinga mfumo mzima wa utaritibu wa posho ulivyo sasa tafakari ya kweli ni kwamba masilahi ya watumishi wa UMMA bado ni madogo sana kwa hiyo Uzalendo wa kweli sio tu kupinga masilahi bora bali serikali iwajibike kikamilifu kudhibiti wizi na ufisadi unaotokana na utaritibu mbaya wa ulipwaji posho , kuongeza makusanyo katika kodi mbali mbali ,kutumia rasilimali za Nchi vizuri ili masilahi ya watu wote Nchi hii yaweze kuwa na tija kwa maisha ya Watanzania na watu wengi waweze kuishi maisha ya faraja na kutimiza malengo yao muhimu ya maisha
Ndio maana nimesema “POSHO SIO DHAMBI ILA POSHO NI DHAMBI PALE POSHO INAPOKOSA UTU.

Nitakuwa ni mtu mwenye mashaka sana kama nikiwaza kuwa masilahi duni na maisha ya kuishi chini ya kiwango ni Uzalendo , Sasa Wabunge mkitaka msipigwe mawe barabarani ,msitukanwe , msionekane ni wasaliti wa jamii aliyowachagua , Sasa huu ni wakati wakusema , Mshahara wa Polisi ,Magereza,JWTZ, Walimu, Makarani Mahakamani na hata sekta zote za Serikali na Binafsi masilahi ya mishahara yao yaongezwe kwa asilimia kama ambavyo mmjiongozea nyie kwenye posho zenu tena zinazohusu siku moja tu lakini wao wanaomba kwa mwezi lakini hawapati. Sasa pamoja na kupinga mfumo mzima wa sera ya posho kama ambavyo Mwenyekiti wetu wa Taifa alisisitiza na kuomba sera hii iangaliwe upya ili kupunguzia Taifa mzigo mkubwa na kuboresha viwango vya mishahara vya watumishi wa UMMA , ni vyema nikarudia kusema kuwa ““POSHO SIO DHAMBI ILA POSHO NI DHAMBI PALE POSHO INAPOKOSA UTU.

Ni kweli gharama za Maisha zimepanda lakini hazikupanda kwa Wabunge tu pia kwa Wananchi wote wanaoishi Tanzania , Hivyo tukiacha ubinafsi tukawajibika vizuri Bungeni kulinda masilahi ya Taifa na kutetea maisha ya Wananchi wetu, bila shaka hata tukionekana tunaendesha magari ya kifahari kama Rolls Royce, Bentley, Benz , hakuna mwananchi hatakeyesema kwa nini Mbunge anaendesha gari zuri kwani kila mtu atakuwa na afadhali ya maisha ktk Nchi yetu.

“ Baba yangu aliniambia “ Watu wengi wanaokwenda Kanisani na Misikitini huwa wanatoa sadaka ndogo kuliko pesa wanayotumia sehemu mbali mbali za anasa ndio maana Taifa lina Bar nyingi kuliko nyumba za Ibada” TAFAKARI

LEMA- MP

Thursday, November 24, 2011

AJALI MBAYA YA LORI DAR ES SALAAM



SIMANZI na majonzi jana vilitawala eneo la River Side, Dar es Salaam baada ya ajali mbaya iliyohusisha lori la mafuta na magari mengine madogo saba kusababisha vifo vya wawili papo hapo na wengine wanne kujeruhiwa vibaya. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alisema ajali hiyo ilitokea majira ya saa saba mchana na kwamba maiti na majeruhi wote walipelekwa Hospitali ya Wilaya ya Ilala, Amana.

Lori la mafuta aina ya Marcedes Benz la Kampuni ya Dalbit lililokuwa likielekea Buguruni liliacha njia na kuyagonga magari saba yaliyokuwa kwenye foleni ya kuelekea Ubungo. Magari mengine yaliyohusika katika ajali hiyo ni Toyota Noah, BMW, Toyota Canter na Toyota Corolla nne. Mmoja wa waliofariki dunia ni mama mmoja ambaye mwili wake ulitenganishwa kabisa na kichwa baada ya gari alilokuwemo kukandamizwa na lori hilo.

Habari kutoka eneo la tukio, zilieleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni lori hilo kuacha njia, baada ya dereva wake kutaka kumkwepa mtembea kwa miguu ambaye alielezwa kuwa ni mama mjamzito. Watu hao wawili waliofariki dunia walikuwa kwenye magari tofauti.

Hata hivyo, habari nyingine zinadai kwamba miongoni mwa waliofariki katika ajali hiyo ni mchuuzi kanda za video ambaye alikuwa akitembeza biashara yake katika eneo hilo. Baadhi ya majeruhi walisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa lori hilo la mafuta baada ya dereva wake kushindwa kulimudu alipojaribu kumkwepa mtembea kwa miguu aliyekuwa anavuka barabara.

“Nilikuwa naelekea Ubungo nikiwa katika foleni, mara nikaona lori la mafuta likiwa linahama njia na kuja upande wetu. Baadaye kidogo, sikuelewa tena kilichokuwa kimetokea,” alisema Yahaya Makame.

Makame ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema licha ya kutokea kwa ajali hiyo mbaya, hakukuwa na msaada wowote wa haraka zaidi wa wakazi wa eneo hilo na wapita njia waliojitokeza kushuhudia. “Ajali imetokea saa 7:00 mchana, lakini, waokoaji wanafika saa 8:00.

Muda wote huo watu walikuwa bado wako ndani ya magari hayo wakiwa wameminywa na lori! Kuna usalama hapo kama siyo neema ya Mungu?” Gari la polisi liliwasili eneo la ajali majira ya saa nane mchana kusaidia uokoaji.

Tume ya katiba sio chombo cha serikali-Shivji


TANZANIA ipo katika vuguvugu la katiba mpya ambalo wiki iliyopita lilichukua sura mpya baada ya matakwa ya asasi za kiraia, wabunge wa vyama vya upinzani na wananchi kwa upande mwingine kupitia asasi za kiraia kupuuuzwa na serikali hivyo kuusoma muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba kwa mara ya pili kinyume na ilivyotakiwa.

Wanaharakati, upinzani na asasi za kiraia walikuwa na hoja ya kutaka muswada huo usomwe kwa mara ya kwanza kwa madai kuwa kuna marekebisho ambayo yamefanywa mara baada ya kusomwa mara ya kwanza na kuusoma kwa mara ya pili si kuwatendea haki wananchi.
Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu, Profesa Issa Shivji anasema kitendo cha serikali kuusoma kwa mara ya pili na kupuuza hoja za wadau wengine ni jambo lisilofaa na linaweza kuitumbukiza nchi katika matatizo yasiyo na msingi wowote.

Anasema kinachofanyika sasa ni sawa na kile ambacho kilifanyika mwaka 1977 chini ya mfumo wa chama kimoja cha siasa ambapo Rais wa kwanza, Julius Kambarage Nyerere alichagua Bunge la Katiba ambalo liliwashirikisha wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hakuna tofauti na wakati ule hivyo kuna hatari ya kupata katiba ambayo haina uhalali wa wananchi kwani itakuwa imetungwa na watu wachache hivyo sioni kwanini turudie makosa ya miaka 40 iliyopita, anasema.

Akichambua zaidi hoja yake hiyo, anasema kulingana na muswada huo Rais wa Bara atawachagua wajumbe wa tume 36 na ibara ya sita ya muswada huo inaeleza kuwa Rais atachagua wajumbe wengine kwa kutumia vigezo ambavyo vimetajwa baada ya makubaliano na Rais wa Zanzibar na ni pamoja na vile ambavyo Rais ataona vinafaa.

Shivji anasema hapo kuna utata kwani muswada haupo wazi kueleza Rais ataona inafaa vipi na hilo anasema ni kumpa madaraka makubwa kiongozi huyo wa nchi katika uteuzi wa tume hiyo ambayo kimsingi ni ya wananchi na sio ya chama, serikali wala kikundi kingine chochote.

Uteuzi wajumbe wa Tume
Kulingana na muswada huo, wabunge wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wale wa Baraza la Wawakilishi ambao wapo chini ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), watakuwa wajumbe wa Bunge hilo la katiba.

Wajumbe wengine wanatajwa kuwa ni mawaziri wa katiba wa serikali zote mbili (Bara/Zanzibar), wanasheria wa pande mbili, wajumbe kutoka mashirika 126 ambayo yameorodheswa na kwa hesabu za haraka Profesa Shivji anasema Bunge hilo litakuwa na wajumbe 554.

Profesa Shivji anasema mchanganuo unaonyesha kuwa wajumbe hao wa Bunge la Katiba kati yao 404 watakuwa wa CCM, 124 watatoka Zanzibar na idadi inayobaki ndio wadau wengine. Profesa Shivji anasema idadi hiyo ni kubwa na haiwezi kuleta ufanisi.
Sijui vipi, lakini India ambayo ina watu wapatao milioni 300 Bunge lao la Katiba mwaka 1945/46 lilikuwa na wajumbe 215 tu, anasema Profesa Shivji.

Swali la kujiuliza hivi wabunge wanaotajwa kuwapo katika Bunge la Katiba wanamwakilisha nani? Wananchi si wapo katika Bunge hilo la Katiba? Je, wao wapo kwa ajili ya nani?
Profesa Shivji anasema makundi hayo mawili yaliingia uwakilishi bungeni kwa mujibu wa katiba iliyopo na walienda huko kutunga sheria kwa mujibu wa katiba hiyo na sio kuipindua ili kuwa na katiba mpya hivyo haoni mantiki ya kuwapo kwao.

Mwenyekiti huyo wa Kigoda cha Mwalimu anahoji kuwapo kwa wabunge wa viti maalum wa CCM na wateule wengine kama asasi za kiraia kunatia wasiwasi na hata hizo NGO ambazo amezichagua Rais si vyombo vya uwakilishi wa wananchi.
NGO ni ‘pressure group’ (makundi ya kushinikiza), tusidanganyane na mara nyingi huwa zinawawakilisha wafadhili baadala ya wananchi. Profesa Shivji anauliza wapi ilipo nafasi ya wananchi katika Bunge hilo?

Aidha anasema kifungu kinachotaja kuwa Rais atateuwa wajumbe baada ya makubaliano na Rais wa Zanzibar ni kuhodhi madaraka ya wananchi.
Kifungu cha sita kimeweka vigezo ambavyo Rais atavitumia na maelezo kuwa na wengine watateuliwa kulingana na vigezo ambavyo rais ataona vinafaa kinajenga maswali zaidi kuliko majibu.

Hapo ni sawa na kumpa mtu kitu kwa mkono wa kushoto kisha kumnyang’anya kwa mkono wa kulia, anasema na kuongeza kuwa Rais kutoa hadidu za rejea za tume hiyo ni kuibaka demokrasia.

Hadidu za rejea
Kulingana na muswada huo, Profesa Shivji anasema kuwa hadidu za rejea zinatolewa na Rais kwa kukubaliana na kushauriana na Rais wa Zanzibar na kitu kama hicho kitafanyika pia katika uteuzi wa katibu wa sekretarieti ya Bunge hilo.
Wajumbe wa sekretarieti watateuliwa na Waziri wa Sheria ambaye pia ndiye mwenye dhamana ya kuwalipa na ndiye ambaye atajua kiwango cha posho na stahili zao zingine na baada ya tume kufanyakazi yake watayakabidhi mapendekezo kwa Rais.

Mapendekezo yatakabidhiwa kwa mujibu wa kifungu namba 18 (2) na baada ya kushauriana na mwenzake wa Zanzibar na baada ya kumaliza majadiliano ya sera na utendaji, Rais atamuagiza Waziri wa Sheria kuwasilisha katika Bunge.
Baada ya kupokea, atamuagiza waziri ayatangaze bungeni, je, akishapokea hataweza kubadili Sheria haimzuii anasema Profesa Shivji.

Shivji anasema anadiriki kusema kuwa ni tume ya marais wawili wa Zanzibar na Bara na sio ya katiba na anaeleza hatua ya kwanza katika kuiunda imewaacha wananchi kando hivyo kupotosha mchakato mzima.
Mwenyekiti huyo wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere anasema sekretarieti ni muhimu ni nani anaiteua ni jambo ambalo linahitaji umakinifu mkubwa na anatoa mfano wakati alipochaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Sheria ya Ardhi wakati wa utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi.

Nilipochaguliwa kuwa mwenyekii wa tume ya ardhi na kupewa ofisi Wizara ya Ardhi, sekretarieti ilikuwa itoke Wizara ya Ardhi, watumishi wa wizara ndio walikuwa sekretarieti, mkutano wa kwanza na wa pili tulioufanya, miniti za kikao hazikuchuliwa, hapo nikaona wazi kuwa tume haiwezi kufanyakazi.

Anasema aliona hivyo kutokana na ukweli kuwa huwezi kuwa na seretarieti kutoka wizarani ambao ndio wanaochunguzwa na tume jambo ambalo alililalamikia na kutakiwa kuchagua sekretarieti yake mwenyewe, hali ambayo ilimuwezesha kufanya kazi zake inavyotakikana.
Tume inaundwa na Rais, marupurupu ya tume yanawekwa na waziri, kwa watu waaminifu sina shaka kabisa, lakini haiwezi kuwa tume huru wakati stahili zao zinalipwa na watu wa serikali na kuwa na tume kama hiyo wananchi hawatahisi kama wapo huru, anasema.

Anasema Profesa Shivji kuwa katika kifungu cha 9 (2) na (3) kinaeleza kuwa tume itazingatia misingi kamili ya kitaifa na maadili ya taifa kwa kuhifadhi na kudumisha mambo yafuatayo ambayo ni pamoja na kutoa fursa kwa wananchi kutoa mawazo yao kwa uhuru kwa lengo la kuendeleza na kuboresha masuala hayo.

Upande mmoja unasema wananchi wataweza kutoa maoni yao kwa mambo yote, tume itahifadhi kudumisha mambo hayo ya msingi lakini hata kama mambo ya msingi ndio wananchi wajadili mambo ambayo hawajayataka,” anahoji.
Mapendekezo
Profrsa Shivji anasema Bunge maalum ni chombo muhimu sana katika utunzi wa katiba mpya na linatarajiwa kutoa uhalali wa kisheria na kisiasa hivyo linatakiwa kiwe chombo cha uwakilishi wa moja kwa moja wa wananchi ni vema uangalifu ukawapo na ikatambulika kuwa ni chombo cha wananchi na sio cha umma.

Tume ya katiba ni chombo cha wananchi kiteuliwe moja kwa moja na wananchi bila kujali chama, elimu hadhi na mambo mengine na Mtanzania yeyote ambaye amefikisha umri wa miaka 18 aweze kugombea ujumbe wa Bunge Maalum,” anasema Profesa Shivji.
Anasema Bunge Maalum ni chombo cha wananchi na kura ya maoni ina maana kuwa wananchi wamejadili, wameelewa na wakipotoshwa katika kura za maoni wanaweza kujenga mfumo wa kidikteta.

Ni muhimu sana kutanguliwa na majadiliano ya muda mrefu na ndio maana tulitaka usomwe kwa mara ya kwanza kutoa nafasi ya wananchi kuujadili, lakini muswada huo ambao awali ulisomwa na kufanyiwa mabadiliko umesomwa kwa mara ya pili na mbaya zaidi hata asasi za kiraia tuliupata wiki moja kabla, anasema.

Kuhusu idadi anasema akiwa mwenyekiti wa tume ya ardhi alikuwa na wajumbe 11 na walizunguka nchi nzima, wilaya zote kasoro mbili na anapendekeza wabunge wasizidi 20 na anataka vyuo vikuu na vyama vya kitaaluma kuwa na wawakilishi katika Bunge hilo kwa kuteua watu wawili au watatu ambao wanaona wanafaa kuingia.

Rais anawajibu wa kuchagua wajumbe kutoka katika orodha ndefu ambayo atakuwa ameipata na waziri anaweza kuwa mjumbe wa tume na sekretarieti iundwe na tume yenyewe na wabunge wa bunge hilo la katiba wamchague mwenyekiti wao, malipo na marupurupu yatajwe na sheria yenyewe.
Profesa Shivji anataka asiwepo mtu wa kuwapangia hadidu za rejea wajumbe hao na ziwe kwa mujibu wa sheria zitakazopitoshwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hakuna haja ya hadidu za rejea, majukumu yote ya tume yametajwa sasa kuna haja gani ya hadidu hizo? Tuepuke malumbano na rasimu hiyo itangazwe hadharani kila mwananchi ajue na mwenyekiti wa tume ndiye aiwasilishe rasimu mbele ya Bunge na sio Waziri wa Sheria, anasema.

Kasoro
Kutokana na muundo wa Bunge tulilonalo hao wote wanaingia katika bunge kupitia vyama vyao na mimi ambaye si mwanachama wa chama chochote cha siasa sina uwakilishi katika bunge la kutunga katiba na mbaya zaidi asilimia 62 hadi 63 wanatoka chama kimoja, anasema.

Profesa Shivji anasema Bunge la Katiba linalotarajiwa halina tofauti na lile la mwaka 1977 ambalo lilifanya iwepo katiba ya sasa inayohitaji mabadiliko kwani Baba wa Taifa, Rais Julius Kambarage Nyerere aliteua wajumbe kutoka Bunge la Muungano na wale wa Baraza la Mapinduzi.

Kuhusu kura za maoni, Profesa Shivji anasema itatoa uhalali, wengi wakisema NDIO inakuwa na nguvu za kisheria kulingana na wingi wa kura na haiwezi kuwa na uhalali sawa na ule wa uchaguzi mkuu hivyo inapaswa kuelezwa itakuwa imepita kutokana na wingi wa asilimia ngapi.
Kitendo cha kupitishwa kwa wingi wa kura bila kutaja asilimia ni wazi kuwa kuna hatari ya kupitishwa na watu wachache, anasema.

Mwafaka
Profesa Shivji anasema mchakato wa upatikanaji wa kabisa mpya ni fursa muhimu ya kurejesha mwafaka kwa majadiliano kuliko ilivyo sasa ambako kuna kila dalili za kuelekea katika magomvi na mapambano.

Anatoa mfano wa kile kilichotokea Kenya wakati wa mchakato wa katiba mpya ya nchi hiyo na kinachotokea katika nchi zingine na mbaya zaidi anasema nchini Tanzania hayo yanatokea wakati nchi inatajwa kuwa na mgawanyiko wa udini na ukabila.
Profesa Shivji anataka itumike nafasi ambayo inapotea kuweka dira na malengo ya kitaifa.

TeluuDailies: Himalayan viagra

TeluuDailies: Himalayan viagra

Wednesday, February 23, 2011

Silly Harry...........

Harry alipochoka kufanya kazi zake akazima taa, akambusu mkewe,
akalala na usingizi mzito ukampitia. Mara akamwona mwanamme amesimama

kitandani.

"Toka hapa nani wewe unakuja kitandani kwangu?"

"mimi ni mtakatifu Petro na hapa si kitandani kwako bali ni mbinguni"

"Ina maana nimekufa? Mbona mimi bado kijana? Naomba unirudishe duniani."

"Inawezekana, lakini siwezi kukurudisha kama mtu, labda nikurudishe kama mbwa au kuku"

Harry akakumbuka mbwa anavyopata taabu ya kulinda, "Bora nirudi kama kuku"

Mara akajikuta yuko kwenye banda, akiwa kuku jike na matakoni kunawaka

moto. Akamwona jogoo pembeni, akamwambia shida yake.

"Kaka ninasikia moto matakoni, inakuwaje?"

"Kwani hujawahi kutaga weye?" Jogoo akamjibu kwa maringo.

"Sijawahi"

"Chuchumaa, kamua kwa nguvu yai litoke."

Basi akakamua, yai la kwanza likatoka, akakamua tena yai la pili hilo !

Akiwa anataka kukamua yai la tatu akasikia sauti ya mke wake.

"Harry, pumbavu wewe, unakunya kitandani!"

Friday, May 07, 2010

Mhadhiri Bakari Mohammed wa Mzumbe University amjibu JK kisayansi!

HOTUBA YA RAIS KIKWETE INA UPUNGUFU WA KISAYANSI

* Alitumia jazba, vitisho na kebehi
* Takwimu alizopewa ni “ghushi”
* Hakujibu madai mengine ya TUCTA


Kwa kuwa mantiki ni mtiririko wa hoja zilizopangwa ili kujenga hoja yenye kukubalika; na kwa kuwa sayansi ni elimu inayotokana na uchunguzi, majaribio, vipimo na kuthibitishwa kwa muda uliopo; kwa hiyo basi, hotuba nzuri ni ile inayozingatia kanuni za kisayansi kwa utumizi wa uchunguzi na mantiki. Sayansi lazima itumike kwa kuwa ndiyo inayoweza kuonesha ukweli na kuutenga na uwongo – uwe wa kimaslahi au vinginevyo – hotuba, kwa hivyo lazima isheheni ukweli na uhakika.

Makala haya nayaandika baada ya kuiskiliza hotuba ya Mhashimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete aliyoitoa mbele ya wale waliyoitwa kuwa ni “Wazee wa Dar es Salaam” siku ya Jumanne tarehe 3 Mei, 2010 kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee. Kwa ujumla, ilikuwa hotuba nzuri ya kisanii – kwa jinsi ilivyotumia lugha rasmi, mifano (mbayuwayu na kigong’ona) na vionjo vya lugha ya kwetu.

Mantiki ya jumla ya hotuba ya Rais Kikwete ilikuwa kuijibu TUCTA japokuwa alitumia nafasi hiyo kuzungumzia Mkutano wa Uchumi wa Dunia (World Economic Forum). Pamoja na mambo mengine ya utangulizi, sehemu muhimu na yenye kuhitaji upembuzi makini na wa kisayansi (uchunguzi + majaribio + vipimo + ithibati + mantiki) ni juu ya matumizi makubwa ya jazba, vitisho, kebehi na hisabati ghushi za takwimu zilizotumika katika kujibu hoja moja (kati ya tatu muhimu) zilizotolewa na TUCTA.

Rais Kikwete alitumia mfano wa “Mauwaji ya Wakata-miwa wa Kilombero” yaliyotokea miaka ya 1980 baada ya FFU (Kikosi cha Kutuliza Ghasia, maarufu kama fanya fujo uone) kutumia risasi za moto na kuuwa! Rais aliendelea kusherehesha juu ya madhila yanayoweza kutokea pale wafanyakazi watakapopambana na POLISI. Sidhani kama ni sahihi kudhani kuwa siku zote migomo huandamana na vurugu na/au ghasia zinazoweza kuzaa utumizi wa nguvu za ki-POLISI na hata mauwaji! Ulikuwa mfano mbaya kutoka kwa Kiongozi Mkuu wa Nchi, aliyesheheni “nguvu” za mamlaka ya kutumia vyombo vyote vya ulinzi na usalama. Ushahidi wa hili unajionesha wazi hata pale penye hadhara yenyewe (Diamond Jubilee): ulikuwapo uongozi wa (1) POLISI; (2) MAGEREZA; (3) Usalama wa Taifa; (4) JWTZ; na (5) Askari wa Siri (Secret Police). Kwa ujumla, mkutano ule ulipambwa na kila aina ya vitisho!

Japokuwa Rais ni Kiongozi wa Nchi na ana mamlaka ya kuamuru majeshi (Ibara ya 33(2), Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 [2005]) bado sayansi ya utawala haikubali kwa kiongozi muadilifu anayefuata haki na insafu kwa watu wake kutumia madaraka hayo dhidi ya utashi halali wa umma! Matumizi ya nguvu za ki-POLISI na/au kijeshi yamewahi kuziingiza nchi kadhaa kwenye sintofahamu na/au songombingo za kisiasa, kijamii na kiuchumi – kama tulivyoshuhudia Kyrgyzstan na tunavyoshuhudia sasa Thailand. Nguvu za ki-POLISI na/au kijeshi zitumike kwa hekima na si vitisho kwa raia (hususan wafanyakazi walalahoi – kama wakata-miwa).

Kwa upande wa utumizi wa lugha yenye murua – kiongozi yeyote awaye na mwenye mamlaka ya juu kiutendaji ana wajibu wa kuchagua maneno yenye hekima; kwa kuwa “hekima ni uhuru”! Rais Kikwete ametamka waziwazi kwamba, “…wafanyakazi wanaotaka kugoma waache kazi…kwa kuwa kuna watu wengi wanaohitaji kazi….” Ni ukweli usiyopingika kwamba “soko la ajira” Tanzania limefurika watu wanaotafuta kazi; lakini si kweli kwamba watu wote wanaotafuta kazi wana sifa stahiki kwa kila kazi.

Haitoshi, si kada zote za kazi (ziwe za kitaaluma na/au kimenejimenti) zina wazalendo wa kutosha kujaza nafasi zitakazoachwa wazi kutokana na: (1) wafanyakazi watakaouwawa (kama nguvu za ki-POLISI zitatumika); (2) watakaofutwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za utumishi wa umma; na (3) watakaoacha na kukimbilia ughaibuni [brain drain]. Nadhani hekima ilibidi itumike hapa ili wafanyakazi wasijione wanyonge mbele ya “Mwajiri Mkuu.” Naomba nichukue fursa hii kunukuu maneno ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere aliyoyatoa Dar es Salaam kwenye Sherehe za Mei Mosi mwaka 1974:


Tulipoanzisha vyama vya wafanyakazi, na halafu baada ya Uhuru kwa uamuzi wa Serikali ya TANU, wafanyakazi wa Tanzania wamelindwa wasinyonywe na matajiri wao, watu binafsi, na hata mashirika ya umma. Na ulinzi huo umezidishwa siku hata siku. Kima cha chini cha mishahara kimewekwa na kimekuwa kikiongezwa mara kwa mara. Sasa ni vigumu sana kumfukuza mfanyakazi, na kila mfanyakazi apate heshima yake kama binadamu (Julius K. Nyerere (1974): UHURU NI KAZI, National Printing Company Ltd, Dar es Salaam, ukurasa 15).

Nukuu hii inatufundisha msimamo wa Mwalimu Nyerere juu ya kuwahakikishia wafanyakazi: (1) ulinzi wa ajira zao dhidi ya unyonyaji unaofanywa na matajiri, watu binafsi, na mashirika ya umma (kama PPF); (2) kuweka kima cha chini cha mshahara na kukibadilishabadilisha kila mara kuendana na utashi wa mwendo wa kiuchumi; (3) kuondoa vitisho vya wafanyakazi kufukuzwa na waajiri; na (4) kuwapa wafanyakazi heshima yao kama binadamu [Ibara ya 12(2), Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 (2005)].

Hotuba ya Rais Kikwete imeonesha wazi kuwa leo wafanyakazi wa Tanzania si kama “Enzi za Mwalimu.” Soko la ajira la leo limewapa nafasi matajiri, watu binafsi, mashirika ya umma na Serikali (yenyewe) kunyonya jasho la wafanyakzai, kuendesha vitisho, kulipa mishahara isiyokidhi maisha (na mafao duni ya uzeeni na/au kiinua mgongo), vitisho vya kufukuzwa kazi, na ukosefu wa heshima kwa wafanyakazi! Inawezekana haya ni matunda ya kuliuwa Azimio la Arusha na mahala pake kuliweka “Azimio la Zanzibar!”

Ukiachilia mbali jazba, vitisho, na kebehi vilivyotumika kwenye hotuba hiyo kuna suala la utumizi wa takwimu ghushi (au ghashi). Kwa mujibu wa hotuba yenyewe (ambayo niliisikiliza mwanzo-mwisho), kutangazwa moja kwa moja (mubashara) na vituo vya runinga vya TBC1 na Star TV na kunukuliwa na magazeti kadhaa yakiwamo: Uhuru (ISSN 0876-3896, Namba 20553 la Jumanne tarehe 4 Mei, 2010); HabariLeo (ISSN 1821-570X, Namba 01230 la Jumanne tarehe 4 Mei, 2010); na Mwananchi (ISSN 0856-7573, Namba 03608 la Jumanne tarehe 4 Mei, 2010). Kwa pamoja, japo numerali (nambari) zilizotumika kwenye habari iliyonukuliwa ni tafauti, bado ukweli unabaki palepale juu ya takwimu zilizotumiwa na Mheshimiwa Rais kuwa ni ghushi.

Rais Kikwete, alitoa mfano kwamba Serikali ikitoa kiwango cha shilingi 315,000 (laki tatu na kumi tano elfu) za ki-Tanzania kwa kila mtumishi (mfanyakazi) itabidi iwalipe watumishi (wafanyakazi) zaidi ya 300,000 (laki tatu) wa sekta ya umma shilingi 6.9 trilioni (Mwananchi), shilingi 6.85 trilioni (Uhuru), na shilingi 6,852.93 bilioni (HabariLeo). Kwa ujumla, takwimu zote zilizonukuliwa zinaonesha kuwa gharama ya kuwalipa watumishi (wafanyakazi) wa Serikali wapatao 350,000 (laki tatu na hamsini elfu) hivi ni shilingi za ki-Tanzania trilioni 6.85293 (kwa mujibu wa gazeti la Serikali, HabariLeo). Takwimu hizo za gharama ya mishahara zilitumiwa na Rais Kikwete kulinganisha na makadirio ya mapato ya Serikali kwa mwaka 2010/2011 yanayokadiriwa kufikia trillion 5.7573 (kwa mujibu wa gazeti la Serikali, HabariLeo) na hivyo kuonesha nakisi ya bajeti ambapo Serikali itawajibika kukopa!

Ilinichukuwa muda kukaa na kutafakari juu ya “ukweli” huu wa ki-hisabati. Japokuwa hisabati ni tatizo la taifa, namshukuru Mwenyezi Mungu kwamba nilipata bahati ya kusoma hisabati tangu nilipoanza kufundishwa hesabu za vidole hadi chuo kikuu! Ziwe hisabati za kikwetu (Traditional Mathematics), hisabati za Entebbe (Entebbe Mathematics), hisabati za msingi (Basic Mathematics), hisabati za ziada (Additional Mathematics), hisabati za juu (Advance Mathematics) hata hisabati halisi (Pure Mathematics) haziwezi kukubaliana na udondozi wa ki-takwimu uliyotumiwa kurahisha hoja iliyotolewa na Mheshimiwa Rais! Na tutumie mifano ili kuelezea hoja ya ki-hisabati kwa utumizi wa sayansi ya nambari (observation + logic).

Achilia mbali wafanyakazi 350,000 (laki tatu na hamsini elfu), tuchukue Serikali ina watumishi (wafanyakazi) 400,000 (laki nne). Angalia jedwali lifuatalo jinsi ya udondozi na/au ukokotozi wa kihisabati:


KIKOKOTOZI GHARAMA


IDADI YA WATUMISHI (iliyokadiriwa)


MSHAHARA KWA MWEZI + Bima + Akiba


IDADI YA MIEZI KWA MWAKA


GHARAMA

Mshahara
400,000
315,000.00

12


1,512,000,000,000.00

Akiba (Mifuko ya Hifadhi ya Jamii)
400,000
315,000.00 (15%)

12


226,800,000,000.00

Bima ya Afya
400,000
315,000.00 (3%)

12


45,360,000,000.00

JUMLA
400,000
371,70.00

12


1,783,160,000,000.00



Kama tukichukuwa mshahara kama “kikokotozi cha gharama” pasipokuwapo na 15% ya akiba (kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii – PPF, PSPF, LAPF na NSSF) na 3% ya bima ya afya (NHIF) serikali itatumia shilingi 1.512 trilioni! Huu ni ukweli wa kihisabati kama wafanyakazi 400,000 (laki nne) watalipwa kima cha chini cha mshahara wa shilingi 315,000 (laki tatu na kumi na tano elfu) Serikali itagharamia shilingi trilioni 1.512 na si shilingi trillion 6.85293! Na hata kama tutachukuwa akiba (15%) na bima (3%) ya afya kwa pamoja (na gharama za huduma nyingine – OC) bado gharama haiwezi kuzidi trilioni 2! Huu ni ukweli wa ki-hisabati na si vinginevyo. Kosa kubwa la kihisabati lililofanywa hapa ni kama asilimia 74 (74%) kutoka kwenye ukweli – hili ni kosa kubwa ki-hisabati – ni mara tatu hivi kutoka kwenye gharama halisi!

Inawezekana Mheshimiwa Rais alipewa takwimu ghushi ili kuonesha kuwa watumishi (wafanyakazi) wa Serikali hawana uzalendo kwa kudai mishahara “mikubwa” kuliko uwezo wa Serikali kugharamia mishahara hiyo! Kama ni kweli alipewa takwimu ghushi, basi aliyempa (na/au waliyempa) wanastahili “adhabu” stahiki kwa vile takwimu hizo ndizo zilizomfanya Mheshimiwa Rais kuhamaki na kupandwa na jazba na hata kutoa vitisho na lugha ya kebehi kwa wafanyakazi. Watu wote waliyomdanganya Mheshimiwa Rais hawana budi kushughulikiwa ipasavyo – na kama ni wasomi wa vyuo vyetu vya ndani basi vyuo vilivyowatunuku stashahada na/au shahada hizo havina budi kuwanyang’anya – kwa vile wamempotosha Rais wa Nchi!

Jambo la mwisho kabla sijahitimisha makala haya nimalizie na nukta kwamba Mheshimiwa Rais hakujibu madai mengine “nyeti” na muhimu yaliyotolewa na TUCTA. Ni yale ya kodi kubwa ya mapato (inayotokana na mishahara) na mafao duni ya uzeeni yanayotolewa na mifuko ya hifadhi ya jamii (hususan PPF). Si jambo jema kuukwepa ukweli japokuwa unasemwa na mtu anayeonekana “duni” na “dhalili.” Ukweli utabaki kuwa ni silaha ya jasiri na uwongo ni silaha ya mwoga! Mwalimu Julius K. Nyerere aliwahi kuandika hivi:


Ukweli una tabia moja nzuri sana. Haujali mkubwa wala mdogo; haujali adui wala rafiki. Kwake watu wote ni sawa. Pia ukweli una tabia ya kujilipiza kisasi kama ukipuuzwa…. Ukweli haupendi kupuuzwa-puuzwa... Wakati mwngine, mtu tunayempinga huwa ana makosa kweli, lakini hoja tunazozitoa ni za ki(bi)nafsi na hazihusiani kabisa na hoja zake. Nikisema mbili na tatu ni sita, nakosa. Lakini ni bora kunionesha kwamba pengine nafikiri tunazidisha kumbe tunajumlisha. Ni kweli mbili mara tatu ni sita; lakini mbili na tatu ni tano siyo sita…. Huu ni mfano wa upuuzi; lakini mara nyingi hoja tunazozitumia kuwashawishi watu wakatae mawazo yetu huwa hazihusiani kabisa na mambo tunayoyajadili (Nyerere, J. K (1962): TUJISAHIHISHE, Dar es Salaam, National Printing Company Ltd, ukurasa wa 3).


Nadhani ni wakati muafaka sasa tuukubali ukweli – hali za wafanyakazi wa Tanzania kwenye sekta ya umma na sekta ya binafsi zinahitaji marekebesho yenye dhamira nzuri – na si vitisho na/au utumizi wa takwimu zisizo na ukweli ili kuogopa kisasi cha ukweli. Mwalimu Nyerere aliliona hili na ndiyo maana aliamua kutuachia urithi wa kitabu hiki chenye umri wa miaka takriban sawa na Uhuru wa Tanganyika! Tujaribu kuyaangalia maneno haya ya Mwalimu Nyerere kwa kuyanukuu kama yalivyo:


Makosa ni makosa na dhuluma ni dhuluma, japo watendao makosa hayo au dhuluma ile ni wakubwa au ni wengi. Chama kinachopenda ukweli na haki hakina budi kiwape wanachama wake uhuru na nafasi ya kusahihisha makosa na kuondoa dhuluma. Wanachama hawana budi waone kuwa ni wajibu wao kuutumia uhuru huo, na nafasi hiyo. Wanachama wasiyotumia uhuru huo na nafasi hiyo, kwa sababu ya kuogopa kuchukiwa au kupoteza nafasi zao, wanafanya kosa kubwa la u(bi)nafsi, ambalo ni adui wa haki na ukweli (Nyerere, J. K (1962): TUJISAHIHISHE, Dar es Salaam, National Printing Company Ltd, ukurasa wa 5).


Haitakuwa vema na wala si haki tukiacha kusimamia ukweli. Ili kuogopa ukweli usijilipize kisasi (Nyerere, 1962) hatuna budi kama raia wa Tanzania kusimamia ukweli ili haki itendeke. Asiachwe mkubwa atende makosa huku wananchi wakimshangilia kwa nyimbo za “sema usiogope” na vigelegele vya tangazo la kuwafuta kazi watumishi watakaogoma! Tanzania ni ya Watanzania na itajengwa na Watanzania kama uongozi utazingatia haki, usawa na uadilifu katika matumizi bora ya rasilimali watu na vitu. Maendeleo ya watu hayaji isipokuwa kwa sera na siasa safi isiyokinzana na utashi wa ki-maumbile.

Sidhani kama kuna watumishi wa Serikali wenye kuona “gere” au kuwa na “hiyana” na CCM hata kutengeza “zengwe” lililoitwa agenda binafsi ya uchaguzi 2010! Wafanyakazi waliitumia Mei Mosi 2010 kutoa wito wao wa “Uchaguzi Mkuu 2010 uwe Suluhisho la Kero za Wafanyakazi.” Nadhani huu ni ukweli wafanyakazi wana kero zao pamoja na (1) mishahara isiyokidhi haja, (2) kodi kubwa ya mapato yatokanayo na mishahara, na (3) mafao duni ya uzeeni yanayotolewa na mifuko ya hifadhi ya jamii (hususan PPF) – huu sio upinzani wa kisiasa na wala hauwezi kutumika kama “agenda ya siri” dhidi ya CCM. Tukumbuke Mwalimu Nyerere (1962) aliwahi kuandika hivi:


Pengine kundi “letu” ni sisi Wana TANU, na “lao” ni la wale wasiokuwa Wana TANU. Kwa mfano, baadhi ya Wana TANU husahau kabisa kuwa baadhi ya watumishi wa serikali ni wananchi safi kabisa kama sisi, na pengine kuwazidi wengine wetu. Lakini kwa sababu hawana kadi za TANU, basi, hufanywa kuwa si kitu. Pengine huongezeka kosa lile lile la kuwafanya wao kuwa ni watumishi tu ambao hawastahili heshima yoyote ya utu. Pengine, kwa sababu baadhi yao wanayo elimu nzuri, huongezeka kosa lile la kuwatilia mashaka wenye elimu. Sisemi kwamba huwa hawana budi wahukumiwe kwa makosa yao ya kweli, si kwa kubwagwa tu katika kundi la walaumiwa bila makosa yao wenyewe (Nyerere, J. K (1962): TUJISAHIHISHE, Dar es Salaam, National Printing Company Ltd, ukurasa wa 13).


Nukuu hii ni muhimu kwa wakati huu. Isitokezee Serikali ya CCM ikadhani kuwa watumishi safi ni wanaCCM pekee – hiyo itakuwa kuwahukumu watumishi wengine wasiyokuwa wanaCCM pasipo na haki. Hakuna haja ya kuwatilia mashaka wenye elimu kwa kuwa uzalendo haupimwi kwa kuwa na kadi ya “chama tawala” isipokuwa utumishi uliyotukuka! Mwisho tukumbuke kuwa, “kila raia anastahili fursa na haki sawa, kwa masharti ya usawa, ya kushika nafasi yoyote ya kazi na shughuli yoyote iliyo chini ya Mamlaka ya Nchi [Ibara 22(2), Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 (2005)].

Na asibaguliwe mtu kutokana na itikadi yake ya kidini, kisiasa, kiuchumi au kijamii. Na Mamlaka ya Nchi ihakikishe kuwa, “kila mtu anayefanya kazi (ya halali) kwenye sekta binafsi au ya umma anastahili kupata malipo ya haki [tazama Ibara 23(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 (2005)]. Mwenyezi Mungu Mtukufu azikunjue nafsi zetu na Atupe hekima ili tuwe huru na mawazo ya chuki dhidi wa watu wasiyo na hatia – na tunapohukumu basi tuhukumu kwa haki kwa kuzingatia usawa, insafu na uadilifu.


“TUMEONEWA KIASI CHA KUTOSHA, TUMENYONYWA KIASI CHA KUTOSHA, TUMEPUUZWA KIASI CHA KUTOSHA. UNYONGE WETU NDIO ULIOTUFANYA TUONEWE, TUNYONYWE NA KUPUUZWA. SASA TUNATAKA MAPINDUZI, MAPINDUZI YATAKAYOTUFANYA TUSIONEWE, TUSINYONYWE NA TUSIPUUZWE TENA,” (AZIMIO LA ARUSHA, 1967).



MUNGU IBARIKI TANZANIA WABARIKI NA WATANZANIA


Makala haya yameandikwa na:

Bakari M Mohamed
Mhadhiri Msaidizi
Kitivo cha Biashara,
Chuo Kikuu Mzumbe,
S.L.P 6,
Mzumbe – Tanzania.
Simu ya kiganjani: +255 713 593347
Barua pepe: maligwa1968@yahoo.com , bakari.mohamed@mzumbe.ac.tz

Wednesday, March 24, 2010

• Akabiliana na shinikizo kutoka Kigoma, Geita

UAMUZI wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, kutangaza azma yake ya kufanya kile alichokiita utafiti wa kujua ni jimbo gani agombee kati ya matano aliyoyaainisha unaonekana kumuweka katika mazingira magumu kisiasa; Tanzania Daima limebaini.

Majimbo hayo matano ambayo tayari yanaonekana kuanza kumgonganisha kichwa Zitto kwa upande mmoja na viongozi na wanachama wa kawaida wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa upande mwingine ni Geita, Kahama, Kigoma Kaskazini, Kigoma Mjini na Kinondoni.

Matukio ya hivi karibuni yanayoweza kumuweka njia panda Zitto ni lile la kuwapo kwa taarifa za vyombo vya habari zinazoonyesha kuwapo kwa shinikizo kutoka kwa wazee wa Kigoma anakotoka mwanasiasa huyo kijana la kumtaka aachane na mipango yake ya kutaka kugombea jimbo lolote nje ya mkoa huo.

Habari iliyoandikwa na gazeti moja la kila siku (siyo Tanzania Daima) ambalo kwa muda mrefu sasa limekuwa na mwelekeo wa kumjenga kisiasa Zitto zinaeleza kuwa wazee wa Kigoma wameshtushwa na hatua ya kijana wao huyo kuanza kusaka jimbo la kugombea.

Wakati wazee wa Kigoma wakitoa tamko hilo, habari kutoka Geita zinaeleza kuwa wakazi wa eneo hilo wameanza kuchangishana fedha zinazofikia sh 50,000 zitakazomwezesha Zitto kuchukulia fomu za kugombea huko.

Katibu wa CHADEMA wilayani Geita, Rogers Luhega, aliliambia Tanzania Daima kwa njia ya simu jana kuwa uamuzi wa kumtaka mwanasiasa huyo kugombea ubunge kwao ulijadiliwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji cha jimbo hilo kilichoketi hivi karibuni.

Luhega alisema uamuzi wa kumpendekeza Zitto kuwa mgombea pekee wa ubunge katika jimbo hilo uliwasilishwa ofisini kwake kwa njia ya barua iliyokusanya maoni ya wana CHADEMA kutoka kata 11 zilizomo jimboni humo.

“Haya ni maombi ya kata zote zilizopo Geita ambazo zilifikia uamuzi huo Machi 14 mwaka huu na kutoa mapendekezo haya ambayo pamoja na mambo mengine yanataka Zitto ateuliwe kuwa mgombea pekee,” alisema.

Alibainisha kuwa kutokana na maombi hayo, CHADEMA wilaya imeshamuandikia barua Zitto, yenye kumbukumbu namba CDM/GT/2010 ikimjulisha kile kilichopendekezwa na wanachama.

Akizungumza kwa simu na Tanzania Daima jana, Zitto alikiti kupokea barua hiyo na mara moja akawataka wana CHADEMA hao wa Geita kuwa na subira.

“Tayari nimeipokea barua ya kuombwa kuwa mgombea pekee nafasi ya ubunge jimbo la Geita mjini kupitia CHADEMA, nafurahi kwa heshima hii, siwezi kukataa lakini ninachowaomba wakazi wa Geita ni kuwa na subira ili nikamilishe taratibu zote ndani ya chama,” alisema Zitto.

Zitto alisema jambo hilo ni kubwa na si busara kulitolea kauli au uamuzi katika kipindi hiki ambacho bado hajaamua ni jimbo gani anapaswa kuwania ubunge.

Alibainisha kuwa alikuwa akikusudia kutoa uamuzi wake Jumamosi hii ya Machi 27 wakati wa mkutano wa Kamati ya Utendaji ya CHADEMA uliopangwa kufanyika mkoani Dodoma.

Jimbo la Geita ambalo linaongozwa na Ernest Mabina kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kipindi cha miaka 10 katika siku za hivi karibu limeonekana kuwa na ushindani mkubwa kati ya CCM na CHADEMA.

Umaarufu wa Zitto katika majimbo ya Geita na Kahama yenye utajiri wa dhahabu, kwa kiwango kikubwa yalijengwa tangu mwanasiasa huyo alipoibua kashfa ya mkataba wa madini wa Buzwagi miaka mitatu iliyopita.

Hata hivyo, nafasi ya Zitto kutoa uamuzi huo Jumamosi hii ni finyu kutokana na chama hicho kufikwa na msiba wa kiongozi wake wa juu, Mzee Christopher Ngaiza, aliyefariki Nairobi, Kenya mwishoni mwa wiki.

Hatua ya Zitto kulazimika kusaka jimbo la kugombea na hususan ule wa kuonekana akibadili uamuzi wa kuendelea kugombea Kigoma Kaskazini umekuwa ukichochewa na mabadiliko ya hali ya hewa kisiasa kwa upande wake.

Kiongozi mmoja wa CHADEMA aliyezungumza na gazeti hili alisema, suala la Zitto kubadili mwelekeo wa kutaka kuendelea kuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini kulianza kujengwa miaka takriban mitatu iliyopita alipokaririwa na gazeti hili akisema alikuwa hana mpango wa kugombea ubunge mwaka 2010.

Tamko hilo la Zitto ambalo liliibua mshtuko mkubwa ndani na nje ya CHADEMA, lilifuatiwa na lile lililotolewa bungeni na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akimtaka mbunge huyo kijana kuwa makini asije akashtukia amepoteza jimbo hilo.

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa Pinda alitoa tamko hilo siku chache tu baada ya kufanya ziara mkoani Kigoma ambako pamoja na mambo mengine alizindua barabara muhimu inayopita katika Jimbo la Kigoma Kaskazini.

Mbali ya hayo, kuwapo kwa taarifa kwamba moja ya kata muhimu yenye wapiga kura 15,000 ya Mwandiga iliyoko katika Jimbo la Kigoma Kaskazini itahamishiwa katika jimbo la Kigoma Mjini, kumekuwa kukitajwa hata na Zitto mwenyewe kuwa sababu iliyomfanya afikirie mara mbili mbili kurejea huko.

Kuhamishwa kwa kata ya Mwandiga yenye wanachama wengi wa CHADEMA kwenda Kigoma Mjini kumewafanya wengi kuanza kuona nafasi ya kijana wao kuendelea kuwa mbunge ikihamia pia katika jimbo hilo.

Hata hivyo, habari zinaeleza kuwa, Zitto mwenyewe amekuwa akisita kugombea Jimbo la Kigoma Mjini kutokana na kukwepa kujiingiza katika mzozo wa kisiasa na Mbunge wa sasa wa CCM, Peter Serukamba, ambaye wana uhusiano wa kihistoria wa kifamilia.

Mkanganyiko huo, habari zinaeleza, ulimfanya mwanasiasa huyo aamue kimsingi kulipa jimbo la Kinondoni chaguo lake la kwanza na kuyaacha mengine manne yakifuatiwa kutegemea na upepo wa kisiasa utakavyovuma.

Source: Tanzania Daima

Monday, June 22, 2009

PIGO KUBWA KATIKA MUZIKI WA TAARABU


Mwimbaji wa siku nyingi wa muziki wa Taarab aliyewahi kutamba na kundi la muungano lililokuwa likiongozwa na Mchezea nyoka maarufu Norbert Chenga Nasma Khamis "Kidogo" amefariki dunia leo kwenye Hospitali ya Temeke alikokuwa amelazwa kutokana na kuugua Maralia
Baba mdogo wa Marehemu ambaye amejitambulisha kwa jina la Mzee Kaniki akizungumza na vyombo vya habari nyumbani kwake Kinondoni Sharif Shamba ambako ndiko msiba uliko amesema Marehemu alikuwa na matatizo ya shinikizo la damu tatizo lililokuwa likimsumbua mara nyingi, hata hivyo siku za hivi karibuni alishikwa na maralia na kupelekwa katika Hospitali ya Temeke ambako alilazwa na kukaa hapo kwa siku nne mpaka mauti yalipompata usiku wa kuamkia leo
Nasma Khamins atakumbukwa kwa nyimbo zake nyingi nzuri zilizokuwa zikipendwa na mashabiki wengi wa muziki kama vile "Naona mambo iko huku" wimbo uliovuma sana wakati huo akiwa na kundi la muungano kundi hilo likiwa hasimu mkubwa wa kundi lingine la la muziki wa Taarab TOT, ambapo mwimbaji mshindani wa Nasma alikuwa alikuwa Khadija Kopa Mungu ailiaze mahali pema peponi Roho ya Marehemu Nasma Khamis Kidogo Amin

Thursday, June 18, 2009

Anayetuhumiwa kumiliki mtandao wa zeutamu adakwa


Polisi wa Tanzania kwa kushirikiana na Polisi wa Kimataifa (Interpol),wamefanikiwa kumshika Raia mmoja wa Uingereza ambaye ana asili ya Tanzania Ndg Malecela Peter Lusinde (pichani) mwenye umri wa miaka 39 na kutuhumiwa kwa kuundesha mtandao wa Ze Utamu.Ndugu Malecela ambaye anajulikana pia kwa jina la "Male" ni Mtaalamu wa kompyuta na ana uwezo wa kuzungumza na kuandika Kiingereza,kiswahili na kichina ana makazi katika mji wa Essex nchini Uingereza.

Wataalamu wa Idara ya upelelezi kutoka Tanzania wakishirikiana na wenzao wa Uingereza wamefanikiwa kuonana na Ndg Male na kupata ushahidi wa kutosha kwamba ndiye alikuwa mmiliki wa Mtandao huo.Idara ya Upelelezi na polisi wa Uingereza wameutaarifu Ubalozi wa Tanzania mjini London kuhusu suala hilo.Maofisa Ubalozi Mr.Clement Kiondo na Amos Msanjila wamefahamishwa jambo hilo.Malecela ni Mtoto wa Mzee Job Lusinde ambaye amewahi kufanya kazi kwenye nyadhifa mbalimbali za utumishi wa serikali Nchini Tanzania.

Habari zilizothibitishwa zinadai kuwa Ndg Malecela amerudishwa Tanzania kwenda kujibu tuhuma mbalimbali za kuendesha mtandao uliokuwa unadhalilisha watu,kuna malalamiko 6850 yaliyoandikishwa kulaumu udhalilishwaji wa watu uliofanywa na mtandao huo,Mtandao huo ulisimamishwa mwanzoni mwa mwezi wa pili kwa maombi ya serikali ya Tanzania baada ya kutoa picha ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete,ufuatiliaji uliofanywa baada ya picha hiyo ndio umepelekea kukamatwa kwa Ndg Malecela.

Haijaeleweka wazi Ndg Malecela atashitakiwa kwa sheria gani? Lakini ni wazi kwamba atashitakiwa Nchini Tanzania.Licha ya Ndg. Malecela Polisi wa Upelelezi wamezungumza na Watanzania wengine wawili katika miji ya Wichita na San Diego Nchini Marekani,ambao pia wanahusishwa na Mtandao huo wa Ze Utamu.

Saturday, June 13, 2009

Colonel Moammar Gadaffi

One of them likes to call himself an "emancipator of women". The other likes women to call him "papi". So when two of the world's most flamboyant and eccentric politicians -- the Libyan leader, Colonel Moammar Gadaffi, and Italy's prime minister, Silvio Berlusconi -- met on Wednesday in Rome, women figured large.



The Libyan leader was accompanied by his all-female, 40-strong bodyguard squad, its members dressed in khaki uniforms and red berets. And the schedule for his controversial first visit to Italy included, at his own request, a meeting on Friday with large numbers of Italian women. Very large numbers.

The plan was for "only" 700. But officials said on Thursday that such was the colonel's drawing power the event had had to be moved to a concert hall with a capacity for 1 000.

Berlusconi has had more than a little trouble lately with embarrassing photos. So it must have been with a sinking ­feeling that he watched the Libyan leader descend the aircraft steps with another one pinned to his chest.

The photograph Gadaffi wore to several of the ceremonies on the opening day of his visit did not show young women in underwear by Berlusconi's poolside, let alone a former Czech prime minister in the altogether. But it was discomforting for his hosts all the same: it showed the Libyan resistance leader, Omar Mukhtar, the "Lion of the Desert", on the day before he was hanged by ­Italian colonialists in 1931.

Gadaffi flew in with a 300-strong retinue, on three Airbuses. As ever, he brought with him a giant Bedouin tent, which was erected in a Rome park.

Security for his visit was tight. But that is partly because, while Gadaffi may have bones to pick with Italy, some Italians have bones to pick with him.

Officially on Thursday it was all smiles as the colonel praised Italy for having "turned a page on the past". Relations have improved since Berlusconi's ­government agreed last year to pay $5-billion in reparations for Italy's ­colonial rule. Italy, Gadaffi said, had "apologised, and that is what allowed me to be able to come here today". But not everyone is happy about the visit. Gadaffi is set to encounter protests over a deal that allows Italian patrols to return would-be migrants, including asylum seekers, to Libyan ports. On Wednesday he dismissed claims that the deal prevented asylum seekers from applying for protection, in a way that visibly disconcerted his host, normally a champion of political incorrectness.

"This is one of the lies that is put about," the colonel declared at a joint press conference after his talks with ­Berlusconi. "The Africans do not have problems of political asylum. People who live in the bush, and often in the desert, don't have political problems. They don't have oppositions or majorities or elections."

UGONJWA GANI UNAOMSUMBUA MWANAHARAKATI HUYU



NA HUYU NAYE NININI YUPO KAWAIDA KWELI

THE LOST YA KIBONGO aka MAISHA PLUS




NILIPATA BAHATI YA KUKUTANA NA WALIOKUWA WASHIRIKI WA MCHEZO WA MAISHA PLUS ULIOKUWA UKIRUSHWA NA TELEVISION YA TAIFA HIVI KARIBUNI NA MSHINDI KUIBUKA BWANA ABDUL HAYUPO PICHANI, MSHIRIKI KUTOKA ZANZIBAR

Friday, June 12, 2009

mdau afunga pingu za maisha

wedding cake

anitha akiweka sign mkataba wa maisha na denis

weding day

akiwa na mpambe wake

maandalizi ya kitchen party

hayawi hayawi sasa yamekuwa mdau denis na mywife wake anitha wakimeremeta baada ya kula pingu za maisha.